MwanzoBTC / USD • Sarafu ya dijitali
add
Bitcoin (BTC / USD)
Bei iliyotangulia
94,518.44
Habari kuhusu Utabiri
Habari kuhusu Donald Trump
Kwenye habari
Kwenye habari
Kwenye habari
Kulingana na takwimu
Kuhusu Bitcoin
Sarafu ya Bit ni mfumo wa malipo dijitali ambao unatumiwa na mamilioni ya watu bila msimamizi wa juu kama Benki Kuu ilivyo katika nchi mbalimbali. Sarafu hiyo huweza kutumika kwa kubadilishana na sarafu nyingine, bidhaa au huduma.
Sarafu ya Bit ilianzishwa na mtu asiyejulikana au kikundi cha watu chini ya jina la Satoshi Nakamoto na kutolewa kama programu huria mwaka 2009. Kuanzia Februari 2015, wafanyabiashara zaidi ya 100,000 wanakubali Sarafu ya Bit kama malipo.
Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Cambridge wa mwaka 2017, kuna watu kati ya milioni 2.9 hadi 5.8 wanaotumia malipo dijitali na wengi wao wanatumia sarafu ya bit.
Mara nyingi sarafu ya bit inaitwa "pesa ya dijitali" lakini wataalamu wengi huiona si pesa bali bidhaa ya bahatisho. Paul Krugmann pamoja na wapokeaji wengine wa Tuzo ya Nobel ya Elimu ya Uchumi aliita udanganyifu akiilinganisha na bahatisho la vitunguu vya maua ya tulip huko Uholanzi katika karne ya 17. WikipediaKuhusu Dola ya Marekani
Dolar ya Marekani ni pesa halali ya Marekani. Alama yake ni $.
Dolar ya Marekani inapatikana kwa noti za dola 1, 2, 5, 10, 20, 50 na 100. Kuna pia sarafu ya dola 1.
Dolar moja ina senti 100. Senti huitwa pia "penny" nchini Marekani. Kuna sarafu za nusu dolar, robo dolar na sarafu za senti 10, 5 na 1.
Hadi mwaka 1969 noti ya dolar ya Marekani ilikuwa na ahadi ya kwamba serikali ya Marekani itampatia kila mtu dhahabu kulingana na thamani ya dola hizi akipenda kuzibadilisha.
Usawa huu na thamani ya dhahabu ulifutwa. Leo hii dolar ya Marekani ni pesa ya kuiamini serikali kama pesa zote. Maana yake watumiaji husadiki ya kwamba serikali haitachapisha dola kushinda uwezo wa uchumi na thamani ya bidhaa zilizopo nchini Tanzania.
Tangu mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia dolar ya Marekani imekuwa pesa kuu duniani na sehemu kubwa ya biashara ya kimataifa hukadiriwa kwa dolar hizo. Lakini tangu kupatikana kwa Euro mwaka 1999 umuhimu wa dolar ya Marekani imeanza kupungua polepole. Hata hivyo nchi mbalimbali zimeachana na sarafu zao na kuamua kutumia dolar ya Marekani tu, k.mf. El Salvador. Wikipedia